1. Haloo jisajiri au sign in kwenye forum hii dakika 1 tu ufaidike na mengi Bonyeza hapa Utaweza kuandika mada yako na itajadiliwa
  Dismiss Notice
Dismiss Notice
Unataka kutangaza kwenye blog maarufu zaidi ya 600 Wasiliana nasi whatsapp 0652428852 Utalipia sh. 666 kwa siku

Matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2017

Discussion in 'Jukwaa la elimu Tanzania' started by support, Sep 6, 2017.

Millionaire  Ads
 1. support

  support Support

  Joined:
  Dec 26, 2016
  Messages:
  303
  Likes Received:
  14
  Trophy Points:
  18
  Gender:
  Male
  Kinachotafutwa ni matokeo mazuri ya mtihani wa darasa la saba 2017. Habari zote na habari za mtihani wa darasa la saba 2017 na matokeo yakitoka tunapeana habari kwenye jukwaa letu hili la kizalendo hapa hapa www.millionairebloggers.com. Kila siku tembelea jukwaa letu tujadili maswala ya kielimu nchini kwetu Tanzania.
  [​IMG]
  Hongereni wanafunzi wa darasa la saba 2017 kwa kuanza mitihani yenu ya kumaliza elimu ya msingi leo tarehe 6/9/2017. Hakika hiyo ni hatua kubwa katika maisha watoto wetu wadogo zetu mmeipiga. Huo ndio mwanzo wa elimu kufikia chuo kikuu. Ni mtihani mkubwa sana huo. Hongereni sana watoto wetu na wadogo zetu kwa kuhitimu elimu yenu ya msingi 2017.

  Wazazi na walezi wa watoto hawa wanaoanza mtihani wa darasa la saba 2017 leo mmejipangaje katika kuhakikisha watoto hawa wanapata haki yao ya msingi ya elimu zaidi ya elimu ya msingi?. Huu ni muda wa kutafakari na kujipanga, Hata kama mtoto hatafaulu ni vyema ukimtafutia kitu mbadala cha kumfanya mtoto wako asikose kupata elimu ya sekondari au hata uhufundi. Namaanisha mtoto huyo aliyehitimu darasa la saba asiishie hapo na kurudi nyumbani kutumikishwa katika kazi za vibarua kama kumtafutia kazi ya mfanyakazi wa ndani "house girl" au house boy au kumpa maji na barafu akauze mtaani. Huo ni unyanyasaji wa watoto.

  Walimu wetu mmmefanya kazi kubwa kuelimisha watoto hao tangu wamekuja kuripoti shuleni wakiwa chekechea wanatokwa na kamasi tu, mmmekuwa zaidi ya wazazi kwakua mlikaa na watoto muda mwingi mkiwafunza maadili na maarifa mengine ya maisha. Tunawashukuru walimu wetu na tunaomba muendelee na moyo huo huo. Millionairebloggers.com inawatakia wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba mafanikio mema katika kufanya mtihani wa darasa la saba 2017
   

Share This Page

Millionaire  Ads
Millionaire  Ads